Msaada wa IOM kunusuru wakimbizi wanaopitia ziwa Albert Uganda

Image

Msaada wa IOM kunusuru wakimbizi wanaopitia ziwa Albert Uganda

Wahamiaji na Wakimbizi

Katika kuhakikisha usalama wa wakimbizi wanaotoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na  kuingia Uganda kupitia Ziwa Albert, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), kwa ufadhili wa mfuko wa Umoja wa Umoja Mataifa wa misaada ya dharura (CERF), limetoa vifaa kwa polisi wanamaji wa ziwa hilo. 

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi wanmaji wa Uganda katika sherehe iliyofanyika kwneye mapokezi ya wakimbizi ya mwalo wa Sebagoro wilayani Kikube.

Vifaa hivyo vya kuokoa maisha ambavyo vimegharimu dola 20,000 ni pamoja na maboya 315 ya kujiokoa, radio saba za mawasilaino na tochi 50 maalum za kumulika majini .

Ali Abdi ni Mkuu wa Ujumbe wa IOM Uganda.

(Sauti ya Ali Abdi)

Tunataka kuhakikisha kwamba wakati wasaka hifadhi wanapokuja wanasafiri kwa njia salama na ya ubinadamu. Kwetu usalama ni jambo na kwanza kwani hali ya hewa yaweza kubadilika wakati wowote, kwa hiyo ni lazima wawe tayari kwa hayo yote”

Mwaka 2014, wakimbizi zaidi ya 100 walizama katika ziwa Albert na tangu kuanza kwa mwaka huu  takriban wakimbizi  20 wakiripotiwa kupoteza maisha yao.

Robert Ngabirano ni Mkuu wa Polisi Wanamaji kwenye Ufukwe wa Sebagoro.

(Sauti ya Ngabirano)

Pia alichukua muda kutoa mafunzo kwa wananchi ya jinsi gani ya kujiokoa iikiwa ajli imetokea…

(Sauti ya Ngabirano)