Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wetu, tunu yetu tuwape elimu inayostahili:Tanzania

Elimu ni mojawapo ya haki za watoto. Picha ya UNICEF Tanzania / Robin Baptista

Watoto wetu, tunu yetu tuwape elimu inayostahili:Tanzania

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Wiki ya elimu Tanzania inaadhimishwa juma hili ikibeba kauli mbiu “uwajibikaji wa pamoja katika kutoa elimu bora, watoto wetu tunu yetu”, madhumini ni kuchagiza ufikiaji wa lengo namba 4 la maendeleo endelevu SDG’s lihusulo elimu.

Maadhimisho haya ya wiki ya elimu yaliyoanza Julai 16 na yatakamilika Julai 20 na yanafanyika nchi nzima yakishirikisha pia wadau mbalimbali wa elimu  yakiwemo mashirika ya kitaifa na kimataifa yanayosaidia kusongesha ajenda ya elimu kama shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Mkoani Morogoro Mashariki mwa nchi hiyo John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzaniakidstime FM ametembelea  maonyesho ya wiki ya elimu  ya mradi wa elimu ya awali unaoendeshwa na shirika la Childhood Development (CDO)  kupitia msaada wa shirika la Children in the cross Fire kutoka Ireland.

Mradi huo ni wa elimu kwa njia ya michezo kwa kutumia vitu vya asili kama mawe, visoda, chupa na vitabu vya picha na unashirikisha shule zaidi ya 40 mkoani humo na Kabambala amemuuliza afisa mradi Joseph Machira kwa nini wameanzisha mradi huo

(SAUTI YA JOSEPH MACHIRA)