Hispania yatumiwa zaidi na wahamiaji kuingia Ulaya- IOM
Idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya kupitia baharí ya Mediteranea ikiendelea kupungua, imeelezwa kuwa wahamiaji sasa wanatumia zaidi Hispania kama njia ya kuingia barani humo.
Shirika hilo limesema idadi ya wanaoingia kupitia Hispania imezidi ile ya walioingia kupitia Italia mwishoni mwa wiki likiongeza kuwa zaidi ya asilimia 35 ya wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediteranea wamepitia magharibi mwa bahari hiyo ikiwani mara tatu ya waliosajiliwa kipindi kama hiki mwaka jana.
Akizungumza na wandishi habari leo mjini Geneva Uswisi msemaji wa IOM Joel Millman amesema licha ya idadi ya wahamiaji wanaotumia njia hiyo kuwa kubwa kuliko ile ya kupitia Italia lakini vifo vimepungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.…
(Sauti Joel Millman)
“Watu 7,000 wametumia njia ya hii wakitokea Afrika kupitia upande wa magharibi mwa baharí ya Mediterania hadi Uhispania katika mwezi huu pekee.”
IOM imesema mbali na wahamiaji waliofaulu kufika Ulaya mwaka huu pekee kuwa 50,872 mpaka sasa waliofariki dunia njiani ni 1,443.
Akifafanua hali hiyo amesema watu waliozama mwezi Juni ni 55 na katika kipindi cha Aprili idadi ilikuwa watu 75 .

Amezungumzia pia tukio la jana nchini Libya la watu takriban wananewaliopatikana ndani ya kontena la lori moja wakiwa wamefariki dunia na wengine wakiwa hoi kutokana na kukosa hewa kando ya barabara mjini Tripoli.
Bwana Millman amesema bado kuna utata kuhusu watu hao..
(SAUTI YA JOEL MILLMAN)
“Bado inashukiwa ikiwa watu hao wanane wahamiaji sita na watoto watatu ndio pekee ama wanaweza kuwa ni 11 kwani afisa wetu mmoja aligusia watu 11 ambao waliripotiwa kufariki dunia katika hospitali walikopelekwa wale waliokuwa bado hai ijapokuwa hali yao ya kiafya ilikuwa taabani.”