Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majiko yatumiayo nishati ya jua ni ushindi kwa SDG’s:SCI

Alan Bigelow na Arun Raman wa Sola Cookers International, wakionyesha vifaa vya kupikia kwa kutumia nishati ya jua , kandoni mwa mkutano wa ngazi ya juu wa kisiasa kuhusu SDG's kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York
UN News/Elizabeth Scaffid
Alan Bigelow na Arun Raman wa Sola Cookers International, wakionyesha vifaa vya kupikia kwa kutumia nishati ya jua , kandoni mwa mkutano wa ngazi ya juu wa kisiasa kuhusu SDG's kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York

Majiko yatumiayo nishati ya jua ni ushindi kwa SDG’s:SCI

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Majiko yatumiayo nishati ya jua pekee au sola  kwa ajili ya kupikia ni Ushindi mkubwa katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDGs, limesema shirika la kimataifa linalochagiza matumizi ya majiko ya nishati ya jua , lijulikanalo kama Solar Cookers International (SCI).

 

Alan Bigelow mkurugenzi wa masuala ya sayansi na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa SCI akizungumza na UN News kandoni mwa jukwaa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa kuhusu nishati endelevu kwa wote amesema

(SAUTI YA ALAN BIGELOW)

 “Nishati ya kupikia ni changamoto kwa takribani asilimia 45 ya watu duniani hivi leo, hivyo nishati ya jua inachotoa ni suluhu kwa watu ambao hususaani wanakabiliwa na changamoto kupata nishati ya msingi kwa ajili ya kupikia , sola ni rasilimali ya bure na inaweza kutumiwa na mtu yeyote mwenye fursa ya kupata jua.”

 

Rosle Marie Bazile (Kushoto) na Alan Bigelow kutoka Solar Cookers International (SCI) wakielezea njia tofauti za kupika kutumia majiko ya nishati ya jua au sola , ambayo ni ya gharama nafuu wakati wa HLP
UN News/ Florence Westergard
Rosle Marie Bazile (Kushoto) na Alan Bigelow kutoka Solar Cookers International (SCI) wakielezea njia tofauti za kupika kutumia majiko ya nishati ya jua au sola , ambayo ni ya gharama nafuu wakati wa HLP

 SCI ina washirika zaidi ya 500 katika nchi 135 kote duniani, moja ya nchi ambazo zinanufaika na mradi huo ni Haiti, Rose Marie Bazile muunguzi na mhadhiri wa chou kikuu katika masuala ya uuguzi na watoto hapa Marekani ni mzaliwa wa Haiti na mwanaharakati wa shirika lisilo la kiserikali la Fuel Direct nchini Haiti, amekuwa akitumia jiko la nishati ya jua tu lisilohitaji betri wala waya kwa miaka mitano sasa

(SAUTI YA ROSE BAZILE)

“Uzoefu wangu wa kupika na sola ni mzuri, ni wa asili, unaolinda afya, unaolinda mazingira, kitu kimoja unachoweza kufanya kwa mazingira ni kupika kwa kutumia sola, kunalinda wakati , kunanipunguzia gharama, kunanipunguzia matumizi ya nishati, ni Ushindi kote kote.”

 Akiunga mkono umuhimu wa matumizi ya majiko hayo katika utekelezaji wa SDG’s Bwana Bigaleow amesema yanazingatia herufi tano ambazo ni

 

(SAUTI YA ALAN BIGALOW )

“C-A-R-E-S: C ni  kukusanya mwanga, A- kunyonya mwanga hivyo masufuria meusi ni muafaka zaidi yananyonya mwanga na kuugeuza moja kwa moja kuwa moto, R-kwa kuhifadhi moto huo, E-ya ufanisi na rahisi kutumia, na S-ni salama na endelevu.”

 Pia amesema matumizi ya nishati ya jua yanasaidia katika suala la maji, usawa wa kijinsi ukizingatia wanawake ndio wanaosenya kuni na malengo mengine kama elimu na afya yatasongeshwa zaidi kwa kutumia nishati hii.