Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jua la Sahel Afrika laweza kuzalisha asilimia 70 ya mahitaji ya umeme duniani

Rachel Kyte, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nishati endelevu kwa wote , anaamini kwamba Ukanda wa Sahel uko mbioni kuwa muhimuli wa nishati ya jua.
UN/Daniel Dickinson
Rachel Kyte, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nishati endelevu kwa wote , anaamini kwamba Ukanda wa Sahel uko mbioni kuwa muhimuli wa nishati ya jua.

Jua la Sahel Afrika laweza kuzalisha asilimia 70 ya mahitaji ya umeme duniani

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Ukanda wa Sahel barani Afrika umeelezwa kuwa mbioni kujikomboa na changamoto ya nishati kuanzia mijini hadi vijijini. Hii ni kutokana na mpango mpya wa Umoja wa Mataifa ambao lengo ni kutumia rasilimali kubwa ya asili ukanda huo ambayo ni jua, kuzalisha umeme kwa matumiazi ya majumbani na shughuli zingine , sio tu Sahel peke yake bali Afrika nzima na zaidi.

Takriban asilimia 70 ya mahitaji ya umeme duniani yanaweza kutolewa kwa kuvuna nishati ya jua kali liwakalo Ukanda wa Sahel barani Afrika. 

Hayo ni kwa mujibu wa mpango mpya wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya ukanda wa Sahel uliozinduliwa hivi karibuni kwa lengo la kuchapuza ushirikiano wa mafanikio na amani ya kudumu kwa nchi 10 zinazounda Ukanda huo.

Rachel Kyte, ni mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya nishati endelevu kwa wote , anaamini kwamba Sahel iko katika mabadiliko ambayo nishati ya jua inaweza kuzalisha umeme katika ukanda huo na hata kwa jamii za  nje ya ukanda.

Paneli za sola ambazo zimetegwa tayari kukusanya nishati hiyo endelevu.
Shutterstock
Paneli za sola ambazo zimetegwa tayari kukusanya nishati hiyo endelevu.

Amesema nishati, ambayo kifedha na kiteknolojia tumeshindwa kuivuna katika historia ya binadamu hadi sasa ambapo tunaweza, swali ni jinsi gani tutaweza kuivuna nishati hiyo kwani kuna uwezekano wa kuweka mashamba ya sola kuvuna jua litakalotoa nishati kwa sehemu kubwa ya Afrika zaidi ya Sahel na kuwasaidia watu wa eneo hilo kuitumia rasilimali hiyo muhimu walioyonayo.”

Bi. Kyte anasema  maono ya mpango huo “ni kwamba tunaweza kutumia nishati ya jua kuboresha mavuno ya kilimo, kusukuma maji kwa matumizi ya kilimo, hali itakayowawezesha kuinua kipato ambacho kitawawezesha kuwekeza kwenye vitu vingine zaidi.

Na kuhusu gharama anasema kuwa “gharama za vifaa vya sola imeshuka kwa zaidi ya asilimia 70 na bei za betri na vifaa vingine pia imeshuka , na hivyo kama tunavyoanza kuona husuan Afrika Mashariki na pia sehemu zingine kama Nigeria na kwengineko soko linakua kwa mifumo ya nyumbani ya sola na watu wa kipato cha chini wanaweza kumudu kwa mfumo wa “lipa kadri utumiavyo.”

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unachagiza kuhakikisha nishati kwa wote ifikapo 2030 na mpango huo utalisaidia bara la Afrika kutimiza ndoto hiyo

Usafishaji wa paneli za sola ili ziweze kuendelea kufanya kazi vizuri.
Dana Smillie / Benki ya Dunia
Usafishaji wa paneli za sola ili ziweze kuendelea kufanya kazi vizuri.