Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamiaji si suala geni limekuwepo tangu jadi-Arbour

Uokozi kwa wakimbizi kwenye pwani ya Italia.(Picha:IOM/Francesco Malavolta)

Uhamiaji si suala geni limekuwepo tangu jadi-Arbour

Wahamiaji na Wakimbizi

Mjadala wa sita na wa mwisho wa majadiliano ya mataifa kuhusu mkataba wa kimataifa wa uhamiaji unafanyika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuwasilisha mkataba utakaoratibiwa baadaye mwaka huu.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji, Louise Arbour ameieleza Idhaa ya Umoja wa Mataifa kuwa..

Sauti ya Arbour

“Wafadhili wana imani kuwa wako karibu kufikia mambo ambayo yatashughulikia wasiwasi wa kila mtu kwa hiyo kwa sasa matarajio ni kwamba kutakuwa na makubaliano Julai 13 na hilo ndilo lilikuwa limejadiliwa.”

Bi. Arbour  amesema mkataba utatoa muongozo wa kukabili mizozo mbalimbali kuhusu uhamiaji akiongeza kuwa yatakuwa ni makubaliano kati ya nchi kuhusu namna ya kufaidika na uhamiaji na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake, kwa hiyo..

Sauti ya Arbour

“Changamoto ya namna ya kukabiliana na kumiminika kwa watu katika mazingira ambayo yanatofautiana katika nchi wanakopitia ambazo hazina uwezo wa kukabiliana na hilo- natumai kwamba mkataba utatoa muongozo  wa njia za kukabiliana na hilo.Lakini lengo sio kwa ajili ya kutoa suluhu za hivi sasa lakini lengo ni suluhu za miaka na miaka.”

IOM wasaidia wakimbizi  Libya.
IOM Niger
IOM wasaidia wakimbizi Libya.

 

Aidha ameongeza kuwa suala la ushikiliaji wa wahamiaji na hususan watoto limejadiliwa kwa kina na kuna wasiwasi mkubwa kuhusu madhara ya kushikilia watu walio uhamishoni kwani inawaweka katika hatari zaidi kuliko kuwasaidia.

Kwa hiyo nadhani ni muhimu kwa watu kuelewa kuwa uhamiaji ni kitu. Sio kitu kizuri wala kibaya. Ni hali ambayo imekuwa sehemu ya historia ya mwanadamu.

Kwa kuhitimisha Bi.Arbour ametolea umma wito

“Chukua sekunde na tafakari na ukweli wa kwamba watu wamevuka mipaka, tunazungumza kuhusu uhamiaji wa kimataifa, sio watu kuhama ndani ya nchi yao, uhamiaji wa kimataifa  umekuwa nasi tangu jadi, umekuwa kwa kiasi kikubwa, kitu kizuri kwa ajili ya mahusiano na binadamu, Jamii zetu zimebadilika, zimekua na kuendelea vizuri kwa ajili ya mabadilishano ambayo yamekuwepo baina ya jamii. Bila shaka inatoa changamoto nyingi. Ni ngumu sana kwa watu kutoka waliko na motisha wa kufanya hivyo ni ngumu kuelewa na ni vibaya kuwaona wahamiaji kama watu walio na ulafi kwamba wahamiaji milioni 258 duniani leo ni watu ambao wana ulafi wa kunufaika kiuchumi.”