Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapata changamoto tunaposaka kubadili sheria zinazokinzana na maadili ya kijadi- Liberia

Msichana wa Liberia akiwa na bendera ya nchi yake, akionyesha utaifa wake.
UNMIL Photo/Staton Winter
Msichana wa Liberia akiwa na bendera ya nchi yake, akionyesha utaifa wake.

Tunapata changamoto tunaposaka kubadili sheria zinazokinzana na maadili ya kijadi- Liberia

Haki za binadamu

Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa  imehitimisha hii leo mapitio ya ripoti ya awali ya Liberia juu ya utekelezaji wake wa vipengele vya agano la kimataifa la haki za kiraia na kisiasa nchini.

Akiwasilisha ripoti hiyo mjini Geneva, Uswisi, Jua Nancy Cassell, ambaye ni Naibu Waziri wa Ulinzi na  Usalama wa Umma katika Wizara ya Sheria nchini Liberia, amekumbusha kwamba 2017 ulikuwa ni mwaka muhimu sana kwa Liberia kutokana na mafanikio yaliyopatikana baada migogoro ya muda mrefu.

Ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Liberia (UNMIL) kukamilisha jukumu lake ulinzi wa amani baada ya miaka 14, na  kurejea kwa utawala wa sheria na kuanzisha upya utaratibu wa kidemokrasia. Mafanikio mengine ni makabidhiano ya amani ya madaraka kutoka kwa Rais Ellen Johnson-Sirleaf kwenda kwa  Rais George Manneh Weah ambaye alishinda uchaguzi.

Amesema  serikali mpya imechukua jukumu la  kuchunguza na kufanya marekebisho muhimu ya masuala yanayohusiana na uraia na sheria za umiliki wa ardhi.

Zaidi ya hayo amesema serikali ilifanya jitihada za kimaendeleo katika ulinzi wa amani na uhuru wa kuzungumza na kujieleza pamoja na kushughulikia ukiukwaji mkubwa  wa vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Katika mjadala uliofuata, wataalamu wa kamati walielezea wasiwasi juu ya tofauti kati ya sheria ya kitamaduni ya ndoa na ile ya kimataifa wakisema chini ya sheria ya kitamaduni umri wa ndoa ni miaka 16 na kwamba kwamba kuoa mwanamke zaidi ya mmoja  inaruhusiwa. 

Pia wamehoji juu ya ubaguzi wa aina nyingi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi  na wapenzi ya  jinsia moja, ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana, unyanyasaji wa majumbani, kutohahalisha utoaji mimba, ukosefu wa usawa wa kijinsia katika mchakato wa kisiasa, na sheria za kitaifa.

Akijibu hoja hizo, Bi. Cassell amesema ijapokuwa Liberia inakabiliwa na changamoto katika kutimiza  wajibu wake katika masuala ya  haki za binadamu  hususan pindi ambapo inataka kurekebisha sheria za kimataifa zinazokinzana na maadili na kanuni za kijadi.