Skip to main content

Ukatili dhidi ya raia Sudan Kusini ni wa kutisha- ripoti

Uthibitisho wa ukiukwaji wa haki za binadamu Sudan Kusini (Picha:UNMISS/Nektarios Markogiannis)

Ukatili dhidi ya raia Sudan Kusini ni wa kutisha- ripoti

Haki za binadamu

Wafuatiliaji wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wamebaini ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanyika kwa makusudi dhidi ya raia ikiwemo ubakaji wanawake kwa magenge na watoto wenye umri mdogo hadi miaka minne. 

Ripoti hiyo iliyowasilishwa leo huko Geneva, Uswisi imesema ukatili huo hususan dhidi ya wanawake na watoto umefanywa na majeshi ya serikali na washirika wake pamoja na vijana waliojihami huko jimbo la Unity  nchini Sudan Kusini.

Wachunguzi walibaini kuwa kati ya tarehe 16 Aprili hadi tarehe 24 mwezi Mei mwaka huu, raia wapatao 232 waliuawabaadhi yao wakining’inizwa mitini na wengine kuchomwa moto ndani ya nyumba zao.

Ripoti inaorodhesha suala la unyanyasaji wa kingono kama chombo cha vita ambapo takriban wanawake na wasichana 120 walibakwa na kundi la wanaume, na baadhi ya hao waliobakwa ni mtoto wa miaka minne.

Mwanamke mmoja alikuwa bado anatokwa na damu baada ya kujifungua lakini naye alibakwa.

Wale waliokataa waliuawa kwa kupigwa risasi na wanawake na wasichana wengine 132 walichukuliwa kwa nguvu

Akifafanua ripoti hiyo Juliette de Rivero ambaye ni mkuu wa dawati la Afrika la kamisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema.

(SAUTI YA JULIETTE de RIVERO)

 Matokeo ni makali sana kuna ukatili wa hali ya juu katika vita nchini Sudan Kusini na kile tulichogundua ni kuwa raia wa kawaida walilengwa kimakusudi katika vijiji vya karibu na eneo hili. Kulikuwa na mauaji ya raia kutokana na mashambulio yaliyofanywa kiholela kwa kutumia mizinga katika vijiji na hivyo kusababisha vifo kwa wazee, na wasiojiweza.’’

Akatoa nukuu za baadhi ya waliohojiwa kwenye uchunguzi huo..

(SAUTI YA JULIETTE de RIVERO3)

" Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14  ambaye anasema kuwa atawezaje kusahau harufu ya miili iliyochomwa kijijini mwake au picha za wanawake waliotundikwa juu ya miti baadhi yao inasemekeana walitundikwa mitini  baada ya kubakwa. »

 Kufuatia ripoti hiyo Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ameisihi serikali ya Sudan Kusini ikomeshe mashambulio yote dhidi ya raia wa kawaida na  ianzishe  uchunguzi na kuwawajibisha wahusika pamoja na wale wanaoongoza.

 

 

Tags : SPLA, ubakaji wa wanawake, Unity State, Sudan Kusini.