Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukabila waweza kusababisha vurugu UN

Bango la kutaka watu wakomeshe ubaguzi.
UN Photo.
Bango la kutaka watu wakomeshe ubaguzi.

Ukabila waweza kusababisha vurugu UN

Haki za binadamu

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu   ubaguzi wa zama za sasa ikiwemo ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni Tendayi Achiume amesema athari za ukabila ni sumu, zimetapakaa na zinaweza kusababisha fujo.

Akihojiwa mjini Geneva, Uswisi Bi. Achiume amesema athari zake ni kubwa kwa baadhi ya watu wanauawa kiholela, na wengine hubaguliwa kutokana na dini yao akitoa mfano wa waislamu wa kabila la Rohingya kutoka Myanmar.

(SAUTI YA TENDAYI ACHIUME)

“Watu wasio na utaifa wanapata  shida ya kuweza kupata elimu, ajira pamoja na huduma za kiafya. Pia wanaweza kuhamishwa kwa njia za haramu. Chanzo muhimu cha kutokuwa na taifa ni ubaguzi wa ukoo, kabila pamoja na dini. Kwa hivyo kilichoko ni kwamba makundi yanabaguliwakutokana na kabila yao, rangi pamoja na uasili wao na wakati mwingine dini yao.”

Amebaini kuwa wale waliokabiliwa na hatari ya kushambuliwa au kuuliwa si wayahudi pekee lakini pia kuna na makundi mengine .

(SAUTI YA TEANDAYI ACHIUME)

“Kuna waislamu, na makundi mbalilmbali ya wachache yanayobaguliwa. Kuna wenye ulemavu; wale wachache wenye mielekeo tofauti ambao huenda wakadhuriwa na unazi mamboleo.”

Ameyataka mataifa kuhakikisha kuwa yanaheshimu azma zao za kuleta usawa kwa  watu wote bila kujali rangi, asili au kabila wala dini ya mtu.