Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pedi za Elea ni mkombozi kwa wasichana na wanawake- Bi. Shigoli

Nchini Ethiopia kiwanda kidogo cha kutengeneza taulo za kike na kimesaidia kupunguza madhila kwa wanawake na watoto wa kike. (Picha:©UNICEF/2016/Carazo)

Pedi za Elea ni mkombozi kwa wasichana na wanawake- Bi. Shigoli

Afya

Harakati za kuona kuwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs unagusa maisha ya kila siku ya wananchi hususan wale wa pembezoni na kipato cha chini zinaendelea kushika kasi, na harakati zilizozaa matunda hivi karibuni ni ubunifu wa pedi za kike ambazo zatumika tena na tena huko Tanzania.

Takribani miaka miwili na nusu tangu kuanza kutengeneza pedi za Elea, zinazoweza kutumika tena na tena, kampuni ya Malkia Investment nchini Tanzania imesema mwelekeo wa matumizi ya vifaa hivyo adhimu kwa wanawake na wasichana ni mzuri.

Afisa Mtendaji wa Kampuni hiyo Jennifer Shigoli ambaye mwaka 2017 alishinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya uanzishaji wa biashara zinazofanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, amesema hayo jijini Dar es salaam akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Dar es salamam, Tanzania.

Bi. Shigoli amesema pedi hizo zinakubalika kutokana na vile ambavyo zinatengenezwa akisema…

(Sauti ya Jeniffer Shigoli)

Akaulizwa ni vipi kuhusu shida ya maji katika kufua pedi hizo?

(Sauti ya Jeniffer Shigoli)

Na kuhusu gharama na matumizi yake, Afisa mtendaji  huyo wa Malkia Investment amesema..

(Sauti ya Jeniffer Shigoli)

Jeniffer aliamua kubuni pedi hizo baada ya kampeni  yake ya matumizi salama ya choo katika shule za msingi kubainisha kuwa wanafunzi wengi wa Kike wanakuwa watoro shuleni au wanakosa vipindi kutokana na kukosa pedi wakati wanapokuwa kwenye hedhi.