Kulemaa viungo sio kulemaa akili- Dkt. Sankok
Kuwa na ulemavu wa aina yoyote ile hakumaanishi umelemaa akili na watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa na mchango katika jamii kama walivyo watu wengine wasio na ulemavu amesema Dkt. kutoka jamii ya Wamasai ya Narok nchini Kenya
Huyu ni Dr Helen Sankok mtaalamu wa masuala ya afya na uzazi wa mpango katika jamii ya Wamaasai huko Narok nchini Kenya, ambaye kwa zaidi ya muongo na nusu sasa anaishi na mumewe mwenye ulemavu wa miguu pamoja na watoto wao.
Anasema katika jamii yake bado ni changamoto kubwa kuwakubali watu na hata watoto wanaozaliwa na ulemavu hususan vijijini.
Mtihani huo haukumsamehe Dr. Sanko hasa pale alipoijulisha familia yake anataka kuolewa na mtu mwenye ulemavu wa miguu.
Hata hivyo baada ya jitihada kubwa za serikali, wanaharakati na makundi ya watu wenye ulemavu kuielimisha jamii anasema nuru imeanza kuangaza gizani kuanzia kwa familia yake