Zeid aikumbusha Iran, hata akikosa nini mtoto haistahili kunyongwa

Vitendo vya unyongaji wa watoto wahalifu vinavyotekelezwa nchini Iran ni kinyume na wajibu wa nchi hiyo kama mwanachama wa mkataba wa haki za watoto na sheria za kimataifa kuhusu haki za kisiasa na kijamii.
Hayo yamesemwa leo mjini Geneva Uswisi na Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein kufuatia Iran kutekeleza hukumu ya kifo dhidi ya kijana Aboklfazi Chezani Sharahi, kwa kosa la kumuua mtu mmoja kwa kumdunga kisu.
Sharahi alikuwa na umri wa miaka 15 tu alipohukumiwa kifo na mahakama moja ya nchini humo, na alinyongwa jana Jumatano.
Zeid Al Hussein amelaani hatua hiyo, akisisitiza kuwa kuwanyonga watoto wahalifu ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na mtoto hapaswi kunyongwa hata kama amefanya kosa gani.
Sharahi ni mtoto wa nne kunyongwa nchini Iran tangu tangu kuanza kwa mwaka huuhuku watoto wengine watano walinyongwa mwaka jana.
Zeid amesema kuna taarifa za watoto wengine 85 wanaosubiri kunyongwa na kuongeza , “tunaelewa kuna mtoto mwingine Mohammad Kalhori, hukumu yake ya kunyongwa itatekelezwa wakati wowote lakini naiomba serikali ya Iran kutotekeleza hukumu hiyo na badala yake kuigeuza adhabu ya kifo kuwa kifungo cha maisha.”
Pia kamishna ameelezea wasiwasi wake wa kutokuwepo na uwazi kabla ya kutekeleza hukumu ya kifo nchini Iran akisema kwa kutotoa taarifa za wakati wa kutekeleza hukumu hiyo hakuweki rehani tu roho ya mfungwa bali pia kunawaweka roho juu familia na jamaa zake hali inayosababisha msongo wa mawazo.
Zeid amesema ofisi yake iko tayari kuisaidia serikali ya Iran kufuata wajibu wake kuelekea haki za binadamu na sharia za kimataifa kuhusu haki za watoto waliofanya