Vipepeo vyawapaisha kiuchumi wanakijiji wa Amani Tanga.
Mradi wa vipepeo katika hifadhi ya taifa ya Amani mkoani Tanga nchini Tanzania umekuwa mkombozi mkubwa kiuchumi hususani kwa wanawake wa vijijini.
Katika juhudi za kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma na treni ya maendeleo endelevu yaani SDGs wanawake hao walikata shauri la kutobweteka na kuanza kujishughulisha na biashara hiyo bunifu ambayo sasa imeinua kipato chao na familia zao lakini pia cha jamii na kuupiga kumbo umasikini.
Akizungumza na idhaa ya kiswahili ya Umoja wa Mataifa Mwanaidi Kijazi ambaye ni mhifadhi katika hifadhi ya taifa ya Amani mkoani Tanga , amesema mazingira mazuri na yenye mvuto katika hifadhi ya Amani yanatoa fursa nyingi za kimaendeleo na ujasiriamali ukiwemo mradi wa biashara ya vipepeo.
Sauti ya Mwanaidi
Na je wanawake wanaofanya biasshara hiyo ya vipepeo wanafaidika vipi ?
Sauti ya Mwanaidi
Na wateja wao ni kina nani?
Sauti ya Mwanaidi