Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hongera wanawake wa Saudia huu ni mwanzo tu:UN

Katibu Mkuu Antonio Guterres akisalimiana na Mwana mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman Al Saud,
Picha na UN/Eskinder Debebe
Katibu Mkuu Antonio Guterres akisalimiana na Mwana mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman Al Saud,

Hongera wanawake wa Saudia huu ni mwanzo tu:UN

Wanawake

Hongera sana wanawake wa Saudia kwa mafanikio makubwa mliyofikia. Pongezi hizo zimetolewa leo na

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akikaribisha hatua ya kuwaondolea mafuruku ya kuendesha magari wanawake wa Ufalme wa Saudi Arabia.

Duru za habari zinasema wanawake wa ufalme huo wameanza leo jumapili kuendesha magari kwenda kazini na sehemu mbalimbali baada ya marufuku ya mwaka 1990 kufutwa na Mfalme mwezi Septemba mwaka 2017.

Kupitia taarifa ya msemaji wake, Katibu Mkuu amesema ni matumaini yake kuwa hatua hii mpya italeta fursa  nyingi nyinginezo kwa wanawake wa ufalme wa Saudi Arabia.

 

Image
. Picha: UM/Loey Felipe
Bendera ya Saudi Arabia (kati).

Pia Bw. Guterres amewapongeza wanawake wa ufalme huo kwa juhudi zao zilizowawezesha kufikia hatua hii muhimu ambayo itachangia uwezo wao wa kijamii na kiuchumi na pia kuliletea maendeleo taifa lao.

Pia amesema anasubiri kuona Saudi Arabia ikipiga hatua nyingine mbele kuelekea kuwapa usawa wanawake pamoja na wasichana