Nimepokea kwa hofu taarifa za mlipuko wa bomu Ethiopia:Guterres

24 Juni 2018

Mtu mmoja ameripotiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa  katika mlipuko uliotokea kwenye mkutano wa hadhara wa waziri mkuu mpya wa Ethiopia Abiy Ahmed siku ya Jumamosi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ,amelaani vikali tukio hilo  la ghasia na kusema amepokea kwa hofu kubwa tarifa hizo za kusikitisha.

Bendera ya Ethiopia. Picha: UM/Loey Felipe
Bendera ya Ethiopia. Picha: UM/Loey Felipe

 

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu“ametuma salamu za  rambirambi zake kwa jamaa za marehremu na kuwatakaia ahuweni ya haraka majeruhi wotena kuonyesha mshimanao wake na watu na serikali ya Ethiopia .

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter