Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi kubwa ya wajane duniani ni mafukara

Mmoja wa wamama wajane kutoka Tanzania.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/N.Ngaiza)

Idadi kubwa ya wajane duniani ni mafukara

Wanawake

Katika kuadhimisha siku ya wajane duniani hii leo, Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya kundi hilo ni mafukara.

Takwimu zinakadiria kuwa duniani kuna wajane milioni 285 na kati yao hao milioni 115 hali zao kiuchumi si shwari.

Ni kwa mantiki hiyo Umoja wa Mataifa kupitia wavuti mahsusi wa siku hii unahimiza nchi wanachama kuwa na mipango pamoja na sera za kukomesha mateso dhidi ya wajane.

 

Aisatou Reourey, 52, ana mgahawa katika kambi ya wakimbizi ya Ngam. Mme we na watoto wake 9 waliuawa katika mgogoro Jamhuri ya Afrika ya kati.
Picha: UN Women/Ryan Brown
Aisatou Reourey, 52, ana mgahawa katika kambi ya wakimbizi ya Ngam. Mme we na watoto wake 9 waliuawa katika mgogoro Jamhuri ya Afrika ya kati.

Mathalani inazitaka serikali zisaidie wajane  kuondokana na umaskini, vile vile watoto wao   wapatiwe elimu kama sehemu ya  mkakati wa kuchapuza mafanikio ya  malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Tarehe 21 mwezi disemba mwaka 2010, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuridhia kuanzishwa kwa siku hii ili kutoa fursa ya kuangazia madhila ya wajane katika kona mbalimbali duniani.