Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Polisi wa operesheni za ulinzi wa amani UN wana mtihani mkubwa: Massanzya

Kamishina wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi Tanzania Nsanto Marijani Massanzya akiwa kwenye mkutano wa UNCOPS
Picha/Patrick Newman
Kamishina wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi Tanzania Nsanto Marijani Massanzya akiwa kwenye mkutano wa UNCOPS

Polisi wa operesheni za ulinzi wa amani UN wana mtihani mkubwa: Massanzya

Amani na Usalama

Polisi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wanakabiliwa na changamoto nyingi wakiwa kwenye operesheni za ulinzi wa amani sehemu mbalimbali duniani, lakini kubwa zaidi ni jukumu la ulinzi wa raia , hususani machafuko yakizuka na kushika kasi kwani hawaruhusiwi kubeba mtutu na kupigana na hapo ndio mtihani unapokuja.

Mkutano wa siku mbili wa viongozi waandamizi wa polisi wa Umoja wa Mataifa (UNPOL) unakunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marikani

Mkutano huo umejadili masula mbalimbali kuanzia majukumu, changamoto, jinsi ya kuzitatua, nafasi ya wanawake katika UNPOL na kupambana na unyanyasaji na ukatili wa kingono katika operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Kamishina wa polisi wa operesheni na mafunzo wa Tanzania Nsanto Marijani Massanzya,  anataja moja ya mtihani mkubwa unaowakabili polisi wa kulinda amani kwenye Umoja wa Mataifa wakiwemo wa kutoka Tanzania

(SAUTI YA NSATO MARIJANI MASSANZYA)

Nini suluhu ya mtihani huo

(SAUTI YA NSATO MARIJANI MASSANZYA )

Na je ujumbe gani anarejea nao nyumbani Tanzania?

(SAUTI YA NSATO MARIJANI MASSANYA )