Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikishwaji jumuishi katika hifadhi ya misitu una tija kwa wanavijiji

Wanainchi pamoja na wageni wakiwa katika hifadhi ya Amani, Tanga Tanzania
Pcha/Aris Maro Creative Commons Tanzania
Wanainchi pamoja na wageni wakiwa katika hifadhi ya Amani, Tanga Tanzania

Ushirikishwaji jumuishi katika hifadhi ya misitu una tija kwa wanavijiji

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Warsha ya siku 5 kuhusu elimu ya ulinzi  na uhifadhi wa mazingira inaendelea katika hifadhi ya misitu ya asili iliyoko amani  Mkoani Tanga, nchini Tanzania.

Wanufaika wakuu wa  warsha ni jamii za vijijini ambazo hutegemea mapato yatokanayo na maliasili ikiwemo utalii, uuzaji wa bidhaa za kitamaduni, viungo na kadhalika. 

Jamii hii mara nyingi hukabiliwa na changamoto za kimaendeleo kwa kukosa mafunzo maalum katika shughuli za kuhifadhi misitu.

Mwanaidi Kijazi ni mhifadhi misitu katika hifadhi ya taifa ya Amani mkoani Tanga na pia ni mmoja kati ya wanaohudhuria warsha hii

Sauti ya mwanaidi……..

Na je wanawake waishio katika vijiji vilivyoko kwenye hifadhi ya Amani wanafaidika vipi na uwekezaji huo ?

Sauti ya mwanaidi….

Miongoni mwa watafiti wakuu katika warsha hii ni Irmeli Mustalahti mhadhiri wa masuala ya  sayansi ya jamii na utafiti  katika chuo kikuu cha Eastern  nchini Finland. Katika tafiti mbalimbali za masuala ya uhifadhi walizozifanya Nepal, Mexico na Tanzania wametoa kipaumbele kwa watendaji wakuu, ushiriki na mikakati ya utawala.

Warsha hii inakijita katika  mambo makuu matatu ambayo ni masuala ya kitaasisi, ujumuishwaji na habari.

Upande wa kitaasisi inatoa kipaumbele kwa utekelezaji wa haki za umiliki wa ardhi kwa wanawake, uimarishaji wa utaratibu wa kutatua migogoro katika jumuiya kwa uwazi, kuwezesha mgawanyiko wa faida kwa jamii na kuhakikisha jamii ina rasilimali za kutosha ili kujifunza na kukabiliana na mantiki mpya ya kuongoza rasilimali. 

Kwa  ujumuishwaji ni kuhakikisha ushiriki wa wote katika maamuzi, matumizi ya ardhi na makundi yaliyotengwa, uimarishaji wa mbinu shirikishi za matumizi ya ardhi na usimamizi wa mazingira, kuhakikisha msaada unaoendelea kutoka kwa mashirika ya kitaifa ili kujenga uwezo katika ngazi tofauti za kimataifa

Na katika nyanja ya habari wanajikita na upatikanaji wa habari za matumizi ya ardhi katika ngazi ya mashinani na kuboresha kumbukumbu ya taasisi juu ya usimamizi wa rasilimali za asili katika kiwango cha jamii na wilaya.

Warsha hiyo, iliyoandaliwa na bodi ya uongozi wa masuala ya uhifadhi wa misitu ya asili duniani inayoongozwa na watafiti kutoka chuo kikuu cha  Michigan na Eastern Finland, ilianza miongo kadhaa iliyopita kwa  lengo la kutengeneza mfumo jumuishi katika jamii mbalimbali duniani ili kukabiliana na changamoto za ukataji miti kiholela katika misitu ya asili, usawa wa kijinsia na uwazi.