Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama tumeweza kujenga kituo cha anga cha kimataifa , tunaweza kufanya chochote: Kelly

Kushoto ni Katibu Mkuu za zamani wa Umoja wa Mataifa U Thant(akiwa kati) akiwa na mwana anga  wa kwanza kutoka Urusi Yuri Gagarin (kulia) and Valentina Tereshkova (lkushoto) kulia kabisa ni mwana anga wa zamani wa Marekani, Scott Kelly,
Picha yaUN/YN (kushoto); Scott Kelly/NASA (kulia)
Kushoto ni Katibu Mkuu za zamani wa Umoja wa Mataifa U Thant(akiwa kati) akiwa na mwana anga wa kwanza kutoka Urusi Yuri Gagarin (kulia) and Valentina Tereshkova (lkushoto) kulia kabisa ni mwana anga wa zamani wa Marekani, Scott Kelly,

Kama tumeweza kujenga kituo cha anga cha kimataifa , tunaweza kufanya chochote: Kelly

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Muonekano wa dunia ukiwa katika mamia ya kilometa kutoka anga za mbali unavutia sana amesema Scott Kelly kinara wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya anga , ambaye pia ni mwanaanga wa zamani wa Marekani.

Kelly akizungumza katika jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya amani ya anga za mbali UNSPACE+50 , mesisitiza kuwa dunia tunayoishi ndio dunia pekee tuliyo nayo.
Katika jukwaa hilo linalofanyika mjini Vienna Austria , amesema kupitia "kifaa kimoja, unaona jinsi gani anga ya dunia ilivyo, ni kama mtu anavyoweka filamu hii nyembamba juu ya uso wa sayari yetu na kwa mara ya kwanza unaiona, na unatambua kwamba ni kila kitu kinachotulinda kutoka kwenyeanga za mbali,”
 
Mwana anga wa NASA Scott Kelly akielea wakati wa kutembea angani 21 Desemba 2.0.+1+5 wakati yeye na mwanaanga mwezie Tim Kopra akichomoa vifaa katika kituo cha anga.
NASA/JOHNSON
Mwana anga wa NASA Scott Kelly akielea wakati wa kutembea angani 21 Desemba 2.0.+1+5 wakati yeye na mwanaanga mwezie Tim Kopra akichomoa vifaa katika kituo cha anga.

Hata hivyo amesema licha ya mafanikio ya picha hizo nzuri na maeneo mazuri, kuna sehemu za dunia zikiangaliwa kutoka angani kila mara zinakuwa zimeghubikwa na uchafuzi.
Ameongeza kuwa “binadamu watafika kwenye sayari ya Mirihi ijulikanayo pia kama Mars au katika sayari nyinginezo kwenye mfumo wa jua, lakini kama ni kwa ajili ya kuishi , basi inahitahi tuweze kwanza kuishi vyema hapa duniani.”
Bwana Kelly ambaye alitumia mwaka mmoja katika mfumo wa sayari kwenye anga za mbali za kiomataifa,  ameelezea maishayake ndani ya kituo cha kimataifa cha anga kuwa ni kipimo cha mfumo maalumu, ambao una urefu wa futi 300 na upana wa futi 200 na mfumo huo unazunguka kati ya kilometa 280-460 angani.
Amehamasisha kwa kusema “Kituo cha anga ni kitu kigumu kabisa tunachoweza kufanya, endapo tunaweza kukifanya , basi tunaweza kufanya chochote”

Mkurugenzi wa UNOOSA Simonetta Di Pippo (Katikati Kushoto) akiwa na maafisa kutokashirika la anga la China kwenye sherehe za utiaji sainim muafaka.
UN News/Runa A
Mkurugenzi wa UNOOSA Simonetta Di Pippo (Katikati Kushoto) akiwa na maafisa kutokashirika la anga la China kwenye sherehe za utiaji sainim muafaka.

 “Tunajenga kituo cha anga wakati tunaizunguka dunia kwa umbali wa maili 17,500, katika eneo tupu likiwa na hali ya hewa ya ama zaidi au pungufu ya nyuzi joto 270, hali ambayo ni ngumu sana kwa wana anga na wahusika wote.”
Kelly ameoanisha ujuzi na uvumilivu huu wa binadamu na hali ya changamoto za kukabiliana na kuendelea kuishi na kuwepo kwa sayari dunia akisema ikiwa tunataka kurekebisha matatizo na kuboresha mazingira tunaweza kufanya hivyo kwani anaamini endapo tutaota kuhusu hilo basi tunaweza kutimiza ndoto hizo na la msingi zaidi ni kufanya hivyo kwa pamoja kwa sababu umoja unatimiza ndoto na upeo wake ni angani.

Pia katika jukwaa hilo ofisi ya Umoja wa Mastaifa ya masuala ya anga UNOOSA na shirika la anga la Uchina CNSA walitia saini muafa wa kuimarisha ushirika wao kuhusu matumizi salama ya anga kwa ajili ya maendeleo 
Muafa huo uliosainiwa na mkurugenzi wa UNOOSA Di Pippo na Katibu Mkuu wa CNSA utakuwa ni wa kuzisaidia nchi zingine zinazoendelea kutumia teknolojia kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo endelevu SDG’s.
 
Kinara wa masuala ya anga wa UN Scott Kelly akikabidhi stampu ya kuadhimisha UNSPACE+50 kwa Rais wa Austria , Alexander Van der Bellen.
UN News/Vibhu Mishra
Kinara wa masuala ya anga wa UN Scott Kelly akikabidhi stampu ya kuadhimisha UNSPACE+50 kwa Rais wa Austria , Alexander Van der Bellen.