Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumesikitishwa na hatua ya Hungary kufanya kutokakuwa na makazi ni uhalifu:UN

Mtu asiye na makazi akiwa ameketi kwenye ngazi za duka moja eneo la Manhattan, jijini New York, nchini Marekani
UN/Pernaca Sudhakaran
Mtu asiye na makazi akiwa ameketi kwenye ngazi za duka moja eneo la Manhattan, jijini New York, nchini Marekani

Tumesikitishwa na hatua ya Hungary kufanya kutokakuwa na makazi ni uhalifu:UN

Haki za binadamu

Hatua ya Hungary ya kufanya hali ya kutokuwa na makazi kuwa ni kosa la jinai na  ni ya kikatili na isiyoendana na sheria za kimataifa za haki  za kibinadamu.

Kauli hiyo imetolewa  leo mjini Geneva Uswisi na mwakilisi maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za kuwepo makazi ya kutosha  , Bi. Leilahi Farha.

Katika barua ya wazi kwa serikali ya Hungary,Leilahi Farha,  amesema pendekezo la serikali la kufanyia marekebisho sheria ya makazi ya nchi hiyo,linawafanya watu wasio na makazi kuonekana ni wahalifu wa kosa la jinai. Pia pendekezo hilo linafanya kitendo cha watu kuishi katika maeneo ya wani kuwa ni kinyume cha sheria.

Mwakilishi huyo amesema ," kamwe haikubaliki kwa serikali kushindwa kutekeleza wajibu wake  chini ya sheria za kimataifa za haki za binadamu n na hasa kushughulikia na kuzuia hali ya watu kukosa makazi  na badala yake kuwalazimisha watu wasio na makazi kuishi maisha mabaya na magumu ya kulipa faini ambazo, bila shaka, hawawezi kuzimudu na hivyo kutishiwa kuswekwa rumande."  Ameenda mbali na kuhoji, " nikosa gani  hilo walilotenda wakati wanaishi maisha yasintofahamu ?"

Kwa sasa kuna watu takriban 50,000 nchini Hungary wanaoishi maisha ya kutokuwa na makazi huku theluthi moja kati yao wakiishi katika mazingira mbay na  theluthi mbili wanaishi katika makazi ya dharura

Inaripotiwa kuwa vibanda vya dharura vilivyoko havitoshi kuwapa makazi watu wote wa nchi hiyo wanaohitaji makazi iwe ni kwa muda mfupi au muda mrefu.

Bi Farha amesema endapo mabadilisho hayo ya katiba yatapasishwa, basi Hungary itakuwa imekiuka mkataba wa kimataifa kuhusu haki  za kiuchumi, kijamii, kitamaduni zinazojumuisha pia kuwepo kwa makazi ya kutosha kwa wote. Kwa hivyo ametoa ombi kwa wabunge nchini Hungary kutopitisha rasimu ya sheria hiyo.