Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za binadamu ni muhimu sasa kuliko wakati wowote ule-Šuc

Kikao cha Barazal la haki za binadamu mjini Geneva.
UN/Elma Okic Edit
Kikao cha Barazal la haki za binadamu mjini Geneva.

Baraza la Haki za binadamu ni muhimu sasa kuliko wakati wowote ule-Šuc

Haki za binadamu

Rais wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Vojislav Šuc, amezungumzia hatua ya Marekani kujitoa kwenye chombo hicho akisema ingawa kila nchi ina haki ya kuamua kuhusu uanachama, bado wakati wa sasa ni wa ushirikiano zaidi wa kimataifa na si vinginevyo.

Vojislav Šuc, amesema baraza hilo ni chombo pekee kinachotoa fursa ya  kipekee kusikia maoni tofauti kuhusu haki za binadamu ambayo  mashirika mengine hayawezi kujadili.

Bwana Šuc amesema ikiwa masuala ya haki za kibinadamu hayawezi kujadiliwa katika chumba cha baraza hilo la haki za binadamu, inamanisha hayawezi kujadiliwa kikamilifu popote pale.

Amesema wakati ambapo haki za kibinadamu zikiwa zinakiukwa kila siku ni muhimu itambulike ya kwamba kuwa na baraza lenye nguvu ni jambo muhimu kwa kipindi cha karne ya 21.

Hata hivyo amesema anajivunia kuongoza baraza hilo ambalo kwa kipindi cha miaka 12 iliyopita limeweza kushughulikia masuala mbalimbali ya haki za kibinadamu.

Amesema Baraza hilo hupaza sauti za wanyonge kabla ya mgogoro haujafika mbali na hatua zake huleta matokeo mazuri kwa waathiriwa wengi wa haki za kibinadamu duniani kote ambao baraza linawatumikia.