Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres akaribisha kuongeza muda wa usitishaji uhasama Afghanistan.

Baada ya shambilizi la kigaidi nchini Afghanistan
UNAMA/Jawad Jalali (file)
Baada ya shambilizi la kigaidi nchini Afghanistan

Guterres akaribisha kuongeza muda wa usitishaji uhasama Afghanistan.

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anakaribisha tangazo la serikali ya Afghanistan la kuongeza muda wa kusitisha mapigano na kundi la Taliban huku  akihimiza kikundi hilo kuitikia wito wa amani kutoka kwa raia wa Afghanistan  na kufuata nyayo za kusitisha mapigano pia.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Bw. Gutereres amesema, anaamini kuwa suluhisho pekee la vita nchini Afghanistan ni kupitia mchakato jumuishi wa kisiasa.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa upo  tayari kufanya kazi na watu wa Afghanistan, Serikali ya Afghanistan na wadau wote ili kufikia amani ya kudumu nchini   humo.

Aidha Bw, Guterres amehimiza pande zote kinzani  kutoruhusu wale wanaojaribu kuchochea na kuvuruga mchakato wa  amani unaoendelea, huku akilaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika hii leo katika mji wa Jalalabad-Torkham  uliopo Mashariki mwa jimbo la Nangahar ambayo yaliwalega raia waliokuwa kwenye sherehe ya Eid na kukatili maisha ya watu 17 na wengine  zaidi ya 10 kujeruhiwa

Bwana Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na pia serikali ya Afghanistan na amewatakia ahuweni ya haraka majeruhi wa shambulio hilo,

Pia ameitaka serikali kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.