Misaada yahitajika kwa maelfu ya wayemeni

14 Juni 2018

Maelfu ya raia wa Yemeni wapo katika hali ya sintofahamu kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye mji wa bandari wa Hudaydah magharibi mwa nchi hiyo.

Mapigano hayo yaliyoanza jumamosi yamsebabisha ongezeko la mahitaji ya misaada ya kibinadamu.

Akihojiwa kwa njia ya simu na Idhaa ya Umoja wa Mataifa Lise Grande ambaye ni mratibu wa ofisi ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa  nchini Yemen, ambaye amezunguniza hali ilivyo katika mji huo..

“Tangu  mapigano mapya siku mbili zilizopita yaanze,  kumekuwepo ya urushaji wa makombora  na wanajeshi kila mahali , na pia kuna milipuko ukanda wa kusini mwa mji kuelekea kwenye uwanja wa ndege. Na leo mapigano ya ardhini yamezidi kuongezeka ukanda wa  pwani.

Na kuhusu mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo bado yanaendelea kutoa misaada japo hali ya sintofahamu inazidi kuongezeka Yemen, Bi Grande amesema…

“Tunafahamu umuhimu wa kubaki na  kuendeleza misaada ya kibindamu katika hali kama hiii. Mashirika yakibinadamu yamejitolea kuwepo panapokuwa na uhitaji wa misaada ya kibindamu. Hiyo ndio kazi yetu.”

Licha ya kuwepo na  mapigano hayo mapya  katika mji wa Hudaydah, Bi. Grande amesema mashirika ya Umoja wa mataifa jana yalipakua zaidi ya tani elfu 63 za misaada ya kibindamu  ikiwemo chakula, mahitaji ya dharura, maji, dawa kwa ajili ya wagonjwa na mafuta ya taa.

Pia ameongeza kuwa kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu pande zote kinzani, zinatakiwa kuruhusu misaada ya kibindamu kuwafikia  walengwa.

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola bilioni 3 ili kuweza kusaidia mahitaji ya watu milioni 22 ambao ni wahitaji wakubwa wa misaada katika mgogoro huu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud