Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwezi mtukufu wa Ramadhani waleta nuru kwa wakimbizi warohingya

Wakimbizi WaRohingya kambini nchini Bangladesh. Picha: WFP

Mwezi mtukufu wa Ramadhani waleta nuru kwa wakimbizi warohingya

Masuala ya UM

Licha ya ugumu ya maisha mkulima mmoja nchini Bangladesh, bado amekuwa na moyo wa kutoa eneo lake la shamba ili kuhifadhi  zaidi ya familia 71 za wakimbizi 300 wa Rohingya waliokimbilia nchini humo kutoka Myanmar.

Muziki...

Hapa ni katika kijiji cha Jamoli nchini Bangladesh ambapo mkulima Akhter Hossain na mkewe Nargis wamewapokea na kuwapatia mahali pa kuishi  wakimbizi warohingya mashariki mwa nchi hiyo.

Muziki..

Sauti ya Akhter

Bado nahisi kulia nikikumbuka mara ya kwanza nilipokutana na familia hizi. Niliwaona wakilia. Ilikuwa ni moyo wa kibinadamu tu. Tuliwakumbatia watoto katika mikono yetu  wakati nguo zao zikiwa zimelowa na nvua.

Hivi sasa wana madarasa 2 ya kuwafundishia watoto ambapo ,  watoto wake wanaweza kucheza na watoto wa wakimbizi tofauti na walivyokuwa peke yao hapo awali….

Mohammad Kassim ni mmoja wa wakimbizi  walionufaika.

Sauti ya Mohammad

Ni raha iliyoje kukaa katika eneo la kaka yangu Akhter. Ni kama tunaishi huko kwetu  Myanmar …..Ndani ya muda mfupi tu upendo kati yetu unazidi kukua, mpaka tumesahau kwamba hatupo nyumbani kwetu.

Muziki...

Kwa kuwa sasa ni mwezi mtukufu wa Ramadhani, ukaribu kati ya jamii ya wenyeji wa Bangladesh na wakimbiziwarohingya, uliwezesha familia ya Akhter kuandaa futari ya pamoja na wakimbizi ikiwa ni ishara ya mshikamano na wageni hao kutoka nchi jirani.