Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ingawa tuna ulemavu serikali ya Kenya inachukua hatua- MUKOBE

Mtafisiri wa  lugha ya alama akiwa katika kikao maalum cha watu wenye ulemavu kuhakikisha watu wenye uziwi hawapitwi  na yanayoendelea kwenye kikao
UN News Centre/Stéphanie Coutrix
Mtafisiri wa lugha ya alama akiwa katika kikao maalum cha watu wenye ulemavu kuhakikisha watu wenye uziwi hawapitwi na yanayoendelea kwenye kikao

Ingawa tuna ulemavu serikali ya Kenya inachukua hatua- MUKOBE

Haki za binadamu

Mkutano wa kimataifa wa watu wenye ulemavu ukiendelea kwenye makao makuu   ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, Kenya inaendelea kuchukua hatua kujumuisha kundi hilo kwenye nyanja mbalimbali ili waweza kukabiliana na changamoto.

Kauli hiyo ya Kenya imetolewa na Josephta Oyeza Mukobe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Urithi wa kitaifa alipohojiwa na idhaa hii kandoni mwa mkutano huu.

Bi. Mukobe ambaye naye pia ana ulemavu wa viungo amezungumzia kwanza changamoto za watu wenye ulemavu nchini mwake.

(SAUTI YA JOSEPHTA MUKOBE)

Hata hivyo pamoja na changamoto hizo Bi. Mukobe amesema kuna mikakati ya serikali ya kukabiliana nazo.

(SAUTI YA JOSEPHTA MUKOBE)