Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres atiwa hofu na mashambulizi Idlib Syria, atka uchunguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia katika mkutano wa amani endelevu.
UN Photo/Evan Schneider
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia katika mkutano wa amani endelevu.

Guterres atiwa hofu na mashambulizi Idlib Syria, atka uchunguzi

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyoarifiwa kulenga Kijiji kimoja huko Kaskazini mwa Idlib nchini Syria wiki iliyopita, na kukatili maisha ya watu kadhaa wakiwemo watoto.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake bwana Stephane Dujarric, Katibu Mkuu ametoa wito wa kufanyika uchunguzi dhidi ya mashambulizi hayo hususan madai kwamba kulikuwa na shambulio la pili ambalo liliwalenga wafanyakazi wa huduma ya kwanza , ili kuhakikisha kuna uwajibikaji kwa wahusika.


Guterres amekumbusha kwamba Idlib ni semu ya eneo la usitishaji uhasama kwa mujibu wa muafaka wa Astana na hivyo ametoa wito kwa wadhamini kutimiza wajibu wao.


Katibu Mkuu ameelezea pia madhalila ya watu takkriban milioni 2.3 waishio jimbo la Idlib, ambao asilimia 60 kati yao ni raia waliotawanywa na machafuko kutoka sehemu nyingine na hivi karibuni Ghouta Mashariki.


Guterres ametaka kusitishwa mara moja kwa uhasama na kuzitaka pande zote kuheshimu wajibu wao chini ya sheria za kimataifa ikiwemo kuwalinda raia na miundombinu yao.
TAGS: Idlib, Syria, Mashambulizi, Antonio Guterres