Wakimbizi Nyarugusu msitoke kambini bila vibali- Kamishna Makakala
Wahamiaji na Wakimbizi
Wakimbizi wanaoishi kwenye kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma nchini Tanzania wametakiwa kuzingatia kanuni za kuwepo kwenye eneo hilo ili kuepuka mkono wa sheria.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini Tanzania Anna Peter Makakala amesema hayo alipozuru kambi hiyo inayohifadhi wakimbizi ambao idadi kubwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Burundi.
(Sauti ya Anna Peter Makakala)
Takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR zinaonyesha kuwa kambi hiyo ina zaidi ya wakimbizi 134,000.