Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbinu muafaka zahitajika kujumuisha katika jamii watoto walioshiriki vita vya silaha

Askari watoto nchini DRC.Umoja wa Mataifa wataka mataifa yote kuafiki kutowatumia watoto katika migogoro ya kijeshi.
UN Photo/Marie Frechon
Askari watoto nchini DRC.Umoja wa Mataifa wataka mataifa yote kuafiki kutowatumia watoto katika migogoro ya kijeshi.

Mbinu muafaka zahitajika kujumuisha katika jamii watoto walioshiriki vita vya silaha

Haki za binadamu

Mkutano maalum unafanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New York Marekani ili kujadilia mbinu muafaka  za kusaidia kuwajumuisha katika jamii watoto walioshiriki migogoro ya silaha na kuepusha migogoro zaidi.

Lengo la mkutano huo uliowaleta pamoja wadau mbalimbali akiwemo mwakalishi wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye migogoro ya silaha ni  kutathmini mpango wa miaka mingi wa kupigania haki za watoto ambao wamekuwa wanahusishwa katika migogoro ya silaha dunaini pasi ridhaa yao.

Mbinu hizo zitawasaidia watoto hao  kuweza kuishi maisha salama na kukubalika na changamoto katika jamii baada ya kushiriki katika migogoro.

Mmoja wa askari watoto wa zamani akiwa na umri wa miaka kumi na miwili tu alipojiunga vitani ni Alfred Orono Orono,hivi sasa  ni afisa anaehusika na kuwalinda watoto katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS nae  aeleza athari za watoto kushiriki migogoro ya silaha

(SAUTI YA ALFRED ORONO ORONO)

Mazungumzo haya pia yana nia ya kutoa picha  kamili ya kampeini hiyo kuwajumuisha watoto katika jamii ambayo imedumu miaka mitano pamoja na umuhimu wake  na jinsi unavyosaidia maisha ya watoto ambao zamani walikuwa wanabeba bunduki ambao unawasaidia.