Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muafaka wa wakimbzi wa Rohingya wafikiwa baina ya UN na Mynmar

Wakimbizi waRohingya wanapoendelea kumiminika Bangladesh, mashirika wahaha kuwasajili. Picha: UNHCR

Muafaka wa wakimbzi wa Rohingya wafikiwa baina ya UN na Mynmar

Wahamiaji na Wakimbizi

Hatimaye makubaliano ya utatu yenye lengo la kufanikisha kurejesha nyumbani wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh. Makubaliano hayo yametiwa saini leo  huko Nay Pyi Taw , mji mkuu wa Myanmar. 

Makubaliano hayo ni baina ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la mpango wa maendeleo, UNDP pamoja na serikali ya Myanmar.

Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Knuts Ostby ambaye ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Mynmar amesema baadhi ya hoja muhimu katika mchakato huo wa kurudi kwa hiyari kwa wakimbizi hao ni mambo ya kuzingatiwa pindi wakirejea nyumbani.

Sauti ya  Knuts Ostby

 Watu hao wanahitaji kuwa na vitambulisho, ni muhimu kuwa na cheti cha uraia ili kujisikia hai katika jamii. Wanahitaji kuwa na uhuru wa kutembea  na kufanya shughuli zao katika jamii.

Hoja nyingine ilikuwa usalama wao wakirejea nyumbani hususan iwapo makubaliano yanagusia suala la serikali kuwahakikishia usalama wa kutosha ?

Sauti ya  Knuts Ostby

Ni muhimu wakawa na fursa ya kuishi kwa amani na majirani zao. Kuna ulazima kuwepo na mchakato wa upatanisho ambao ni sehemu ya programu ya maendeleo. Hili haliwezekani kutatuliwa kisiasa tu bali kimaendeleo.

Makubaliano hayo pia yatoa uhuru kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa kuwapatia misaada ya kibinadamu wakimbizi pindi watakaporejea  jimboni kwao Rakhine na pia kuwasaidia katika mchakato wa ujenzi wa makazi yao mapya.

Serikali kwa upande wake inatakiwa itekeleze mchakato wa kuwapatia vitambulisho vya uraia  pamoja na uhuru wa kuabudu na kufanya shughuli zao za kijamii.

Zaidi ya wakimbizi 700,000 wa rohingya wamekimbilia Bangladesh kuanzia mwezi Agosti mwaka jana kutokana na mashambulizi dhidi yao huko jimboni Rakhine.