Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yalaani shambulio dhidi ya walinda amani Sudan Kusini

UNMISS

UNMISS yalaani shambulio dhidi ya walinda amani Sudan Kusini

Amani na Usalama

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini  UNMISS, umeklaani vikali shambulio dhidi ya walinda amani katika jimbo la Unity.

Kwa  mujibu wa UNMISS  shambalio hilo limetokea  jumatatu  katika sehemu ya Rubkwany, umbali wa kilomita 20 kaskazini mashariki mwa  mji wa Leer wakati Kikosi cha UNMISS kilipokuwa katika doria ya kawaida. Joshua Mmali ni kaimu msemaji wa UNMISS nchini humo anafafanua zaidi kuhusu tukio hilo.

(Sauti ya Joshua Mmali)

Eneo hilo lina kawaida ya kuwa na makundi mbalimbali yanayohasimiana . Je ni kundi gani lililohusika na shambulio dhidhi ya  UNMISS?

(Sauti ya Joshua Mmali)

Ameongeza kuwa  UNMISS imezitaka pande zote husika  kuheshimu watumishi wa Umoja wa mataifa na kuwaruhusukutembea kwa uhuru. Pia imeyataka makundi hayo  kushirikiana na walinda amani katika kuwalinda  raia  na kuunga mkono juhudi za kumaliza machafuko.