Kisichofaa kutumika tena na tena achana nacho :Guterres

5 Juni 2018

Kataa matumizi ya plastiki zinazotumika mara moja na kutupwa, ni kauli ya Umoja wa Mataifa katika siku ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani.

Katibu Mkuu Antonio Guterres katika ujumbe alioutoa jijini New York, Marekani amesisitiza umuhimu wa ulinzi na uhifadhi wa baharí na mito dhidi ya matumizi ya plastiki na hivyo kulinda sayari na viumbe vyote viishivyo ndani yake.

Antonio Guterres

“Sayari yenye afya ni muhimu kwa mustakhabali wenye mafanikio na amani. Sisi sote tuna jukumu la kutekeleza katika kulinda makazi haya tuliyo nayo.”

Na je plastiki zitumiwazo mara moja na kutupwa zinaishia wapi?

 

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP Erik Solheim na Barlozi mwema wa shirika hiilo Dia Mirza katika harakati za usafi wakati wa siku mazingira ambayo yameadhimiwa kimataifa India.
UN Environment/Ishan Tankha
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP Erik Solheim na Barlozi mwema wa shirika hiilo Dia Mirza katika harakati za usafi wakati wa siku mazingira ambayo yameadhimiwa kimataifa India.

Antonio Guterres

 Kila mwaka zaidi ya tani milioni 8 za plastiki huishia kutupwa baharini. Chembechembe za plastiki baharini hivi sasa zinazidi idadi ya nyota katika anga letu. Kuanzia visiwa vya mbali hadi Artic, hakuna mahali ambapo hapajaguswa.

Guterres anasema ifikapo mwaka 2050 bahari zote zitakuwa na plastiki nyingi zaidi kuliko samaki endapo hakuna jitihada za kupunguza matumizi ya plastiki.

Antonio Guterres

 “Kwa pamoja tunaweza kubadilisha njia kuelekea ulimwengu safi wenye kujali mazingira. Kataa matumizi ya plastiki zinazotumiwa mara moja  na kutupwa.”

Kimataifa, maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yamefanyika nchini India ambako Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja waMataifa, Erik Solheim ameshiriki pia katika shughuli za usafi kwenye maeneo ya Taj Mahal.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter