Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani wa Tanzania auawa CAR, saba wajeruhiwa:UN

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania walio kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.
MONUSCO Forces/FIB-TANZBATT
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania walio kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Mlinda amani wa Tanzania auawa CAR, saba wajeruhiwa:UN

Amani na Usalama

Mlinda amani mmoja kutoka Tanzania ameuawa na wengine saba kujeruhiwa jana kwenye kijiji cha Dilapoko eneo la Mambarika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Stephane Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa  akitoa tarifa kwa waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo ameelezea kilichotokea na hali ya majeruhi,  Tukio hilo limetokea wakati kikosi cha Umoja wa Mataifa kilichokuwa katika doria kilipovamiwa na wanaodaiwa kuwa wapiganaji waliokuwa na silaha.  Na kwa walinda amani saba waliojeruhiwa mmoja yuko katika hali mahtuti na anapatiwa matibabu katika hospital ya jeshi ya mpango wa Umoja wa Mataifa mjini Bangui pamoja na majeruhi wengine watatu ambao hali yao ni mbaya, na majeruhi wengine watatu waliosalia wanatibiwa Berirati.

Ameongeza kuwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio huo. Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitafuata baadaye.