Badala ya beseni la chakula, watoto DRC wabeba beseni la mchanga
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vita na janga la kibinadamu nchini humo vimesababisha watoto kulazimika kufanya kazi ili waweze kutunza familia zao. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vita na janga la kibinadamu nchini humo vimesababisha watoto kulazimika kufanya kazi ili waweze kutunza familia zao. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
Ni msururu wa watoto wakiwa wamebeba magunia, makarai na magudulia yaliyojaa mchanga wakitoka fukwe za ziwa Tanganyika eneo la Kalemie, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC
Watoto hawa ni miongoni mwa mamia kwa maelfu ya watu ,wazee kwa watoto na wake kwa waume wanaohangaishwa na migogoro inayokumba jimbo la Tanganyika lililo mashariki mwa nchi hiyo.
Umaskini, njaa na magonjwa vinawakabili licha ya kamisaada kama vile kutoka shirika la kuwahudumia wakimbizi-UNHCR bado watoto hawa wanaendelea kupambana ili waweze kuishi.
Mmoja wao ni Françoise Asani Philippe.
Watoto hawa wa kike na wa kiume baadhi yao wakiwa na umri wa miaka mitano, badala ya kubeba beseni au sahani za vyakula, wanabeba mabeseni ya mchanga ili apate kipato. Na hufanya kazi hii tangu saa kumi na nusu alfajiri.
Mchanga huu sana sana hutumiwa kujengea nyumba na malipo kwa watoto ni gharama ndogo. Mtoto hupewa sentí 30 ya dola kwa kila kilo 25 za mchanga anazobeba.
Hapa wazazi hawana la kufanya ila kuwaacha watoto wafanye kazi kama asemavyo baba mzazi wa Francoise, aitwaye Philippe Kika Malisawa.
“ Wazazi wetu hawakutufanyisha kazi kiasi hiki. Tulikuwa tunakaa tu na baba zetu wanatuletea chakula. Lakini sasa kwa sababu hatuna pa kuishi tunateseka tu.”