Wajumbe walilia amani Sudan Kusini

21 Mei 2018

Wajumbe na viongozi wa kidini kutoka Sudan Kusini, wanaohudhuria mkutano wa ngazi za juu wa jukwaa la kuongeza matumaini ya amani nchini mwao, wamejikuta wakibubujika machozi kutokana na mateso waliyoshuhudia nchini mwao.

Vilio hivi vya wajumbe wanaoshiriki kwenye mkutano wa pande zote zinazohasimiana nchini Sudan Kusini, na ni wakati wa mkutano huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, na lengo ni kushawishi pande kinzani Sudan Kusini ziheshimu mkataba wa kusitisha mapigano uliotiwa saini mjini humo mwaka 2015.

Kwa mujibu wa Radio Miraya ambayo ni ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wawakilishi wa wanawake kutoka Sudan Kusini, Amir Deng  na Sarah Nyanek waliwaomba waumini wapige magoti kuombea wanaume na watoto pamoja na jamaa zao waliopoteza maisha yao wakiuliza ni vipi wanaweza kuwashawishi viongozi wa kisiasa nchini mwao walete amani.

Naye Askofu wa kanisa ya Kiinjili huko Akobo, John Jok , alibubujika machozi kutokana na vifo vilivyosababishwa na vita vya kisiasa pamoja na kikabila akisema hajui la kusema,

Ameongeza kuwa alichoshuhudia Akobo ni  mateso pamoja shida ambavyo havipaswi kuendelea.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter