Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila nyuki ni kama Ulimwengu bila ladha tofauti ya chakula

Siku ya nyuki duniani
Picha ya FAO
Siku ya nyuki duniani

Bila nyuki ni kama Ulimwengu bila ladha tofauti ya chakula

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katika maadhimisho ya siku ya nyuki duniani mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la chakula na kilimo duniani  FAO na wadau yameendelea kuweka mkazo katika ulinzi na utunzaji wa nyuki kwa ulinzi wa mazingira na pia matumizi ya binadamu.

Katika kupigia chepuo umuhimu wa wavuvizi, na pia kupunguza vitisho ambavyo wanakabiliana navyo  pamoja na  mchango wao katika  maendeleo endelevu, Umoja wa Mataifa ulichagua  siku ya mei 20 kama siku ya nyuki Ulimwenguni.
 
Nyuki, vipepeo na aina nyingine ya wavuvizi, wana mchango mkubwa katika maisha ya mwanadamu. Chakula ambacho tunachokula, kama vile matunda na mboga, hutegemea moja kwa moja na machango wa nyuki. Dunia bila wavuvizi, ni sawa na ulimwengu bila ladha tofauti ya chakula kama kahawa, chokoleti, matango na mengine.
 
 
Aina nyingi  ya maua  huzalisha  mbegu tu ikiwa nyuki wamehamisha poleni kutoka kiini cha ua moja hadi nyingine .Bila zoezi hilo, maua hayawezi kuchanua au kuzaliana katika mazingira.
 
Nyuki na jamii nzima ya wavuvizi wana  umuhimu  sana kwa uzalishaji wa chakula katika maisha ya binadamu na pia wana mchango mkubwa katika ulinzi wa  mazingira na mifumo ya uzalishaji  katika  kilimo.