Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Poleni wafiwa katika ajali ya ndege Havana: Guterres

Ajali ya ndege
Picha ya UNNews
Ajali ya ndege

Poleni wafiwa katika ajali ya ndege Havana: Guterres

Msaada wa Kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya ndege ya jana tarehe 18 mjini Havana  Cuba na kusababisha maafa kwa raia wengi.

Kupitia msemaji wake, Bwana Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa wote pamoja na serikali ya Cuba wakati huu mgumu ambapo taifa la Cuba linakabiliwa na msiba mkubwa wa kitaifa.

Ndege aina ya Boeing 737-201 ilipata ajali ijumaa , muda mfupi baada ya kuondoka  katika uwanja wa kimataifa wa  Havana  ikiwa safarini kuelekea  katika mji wa  Holguin  mashariki wa kisiwa na  kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Mamlaka za Cuba imezinduwa uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo, huku siku mbili za maombolezo ya kitaifa zikiwa zimetangazwa.