Vikwazo vya kiuchumi Syria ni kigingi kwa misaada ya kibindamu
Mtaalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa asema , vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Syria vinaathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa maelfu ya wathitaji nchini humo.
Bw Idriss Jazairy, aliyemaliza ziara ya siku 4 nchini humo kwa mwaliko wa serikali ya Syria, amesema amebaini kuwa vikwazo jivyo dhidi ya serikai ya Syria kwa namna moaja au nyingine vimekuwakizingiti kikubwa katika ukuajii wa uchumi wa nchini hiyo na pia katika ufikishaji wa misaada ya kibinadamu kwa walengwa.
Katika ripoti yake bwana Jazairy amesema haungi mkono mgogoro wa Syria au vitendo vya kikatili vinavyofanywa na serikali ya Syria, ila kwa mtazamo wa kibinadamu ongezeko la vikwazo vya kiuchumi tangu mwaka 2010 vimechangia sana kuporomoka kwa uchumi na kuaathiri soko la ajira Syria kwa kiwango kikubwa huku mfumuko wa bei ukiongezeka kila uchao na kusababisha theluthi moja ya waSyria kukosa chakula.
Pia amesema anaamini kwamba wadau wote wenye nafasi ya kutoa misaada ikiwemo chakula, huduma ya afya, maji na misaada mingine ya kibinadamu wanayo nafasi ya kujiunga kwa pamoja kuwezesha mahitaji ya kibinadamu kuwafikia watu ambao ni wahitaji .
Mtalamu huyo atarajia kuwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la haki za binadamu mwezi septemba mwaka huu.