Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran sasa rasmi ni mwanachama kamili wa IARC

UN Photo/Loey Felipe
Bendera ya Iran (kati). Picha:

Iran sasa rasmi ni mwanachama kamili wa IARC

Msaada wa Kibinadamu

Iran imejiunga  rasmi na shirika la kimataifa linalotafiti masuala ya saratani IARC

Iran sasa imekuwa nchi ya 26 kuwa mwanachama wa shirika hilo japo imekuwa ikishirikiana na shirika hilo kwa muda mrefu.

Akiikaribisha rasmi leo katika shirika hilo mjini Lyon Ufaransa, Mkurugenzi wa shirika hilo, Dr Christopher Wild amesema kuwa , serikali ya Kiislamu ya Iranimejikita  katika kukuza utafiti wa jinsi ya kuzuia saratani pamoja na mpango wa kudhibiti satarani kwa muda mrefu.

Uanachama wa Iran pia ni ishara ya juhudi za shirika hilo kuwaingiza chamani mataifa shirikishi kutoka maeneo ambayo hayajawailishwa kikamilifu.