Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na Benki ya Dunia zashirikiana kukwamua wahitaji duniani

Mmoja wa wahamiaji waliorejeshwa kwa hiyari kutoka Libya akifanya ujasiriamali. Picha na IOM

IOM na Benki ya Dunia zashirikiana kukwamua wahitaji duniani

Wahamiaji na Wakimbizi

IOM na Benki ya Dunia sasa kushirikiana kwenye maeneo  ya kuboresha  ustawi wa kibinadamu.

Makubaliano yenye lengo la kuchagiza maendeleo na kushughulikia changamoto za kibinadamu duniani yametiwa saini leo huko Geneva, Uswisi kati ya Benki ya Dunia na shirika la uhamiaij la Umoja wa Mataifa, IOM.

Ushirika kati ya pande mbili hizo umezingatia ukweli kwamba majukumu yao katika kushughulikia masuala hayo yanaendana na hivyo pande hizo zikaona ni vyema kuwa kutia saini makubaliano ya maelewano ili kufanikisha dhima hizo.

Mathalani kusaidia kukwamua wahanga wa majanga, kusaka mbinu bunifu za majanga yaliyoota mizizi na pia kutafuta uhusiano kati ya uhamiaji na maendeleo.

Akizungumza mjini Geneva, Uswisi baada ya kutia saini makubaliano hayo Mkuu wa ofisi ya IOM huko Washington, DC nchini Marekani Luca Dall’Oglio amesema makubaliano hayo yataweka mfumo ambamo kwao usaidizi wa kifedha kutoka pande mbili hizo utasaidia mamlaka za kitaifa kutekeleza miradi muhimu.

Wametaja mradi huko Iraq ambao unalenga kuinua kipato cha zaidi ya raia milioni moja kupitia mfumo wa kuwapatia fedha, ajira za mura na huduma nyinginezo.