Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hata wakati wa migogoro zalisheni chakula- FAO

Ufunguzi wa mkutano wa kikanda  wa maafisa wandamizi katika makao maku ya FAO Roma.
Picha ya FAO/Guiseppe Carotenuto
Ufunguzi wa mkutano wa kikanda wa maafisa wandamizi katika makao maku ya FAO Roma.

Hata wakati wa migogoro zalisheni chakula- FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Migogoro imeongeza uhaba wa chakula katika  maeneo ya kanda ya nchi za Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo,  FAO Jose Graziano da Silva  amesema hayo leo mjini Roma, Italia wakati wa ufunguzi wa kikao cha mkutano wa kikanda ulioleta pamoja  mawaziri na viongozi wengine kutoka mataifa zaidi ya 30.

Amesema ili hali hiyo ibadilike ni lazima kuziwezesha jamii maskini, pamoja na zile ya mashambani ili ziweze kujikwamua hususan kwa kuzipatia maji safi.

Mkuu huyo wa FAO amesema kuwa hata wakati wa migogoro, wanaweza kufanya mengi ili mifumo ya kuzalisha chakula ya kila sehemu iweze inaendelea kufanya kazi kama kawaida ili kuleta matumaini kwa watu walioathirika.

Bwana Da Silva amebaini kuwa hadi mwaka wa 2013, eneo la Kaskazini mwa Afrika pamoja na Mashariki ya Kati yamekuwa yanajivunia kipindi cha chakula tele, lakini kuanzia mwaka huo uhaba wa chakula  umeongezeka kwa asilimia 15. 

Amesema hali hiyo imesababishwa baadhi ya nchi katika eneo hilo kukabiliana na migogoro ya muda mrefu.

Kiwango cha ukosefu wa chakula kwa nchi zilizo na migogoro katika eneo la Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, kwa mujibu wa mkuu wa FAO, kimefikia asilimia 28 na hii ikiwa ni mara sita zaidi ya  nchi ambazo hazina migogoro katika kanda hiyo moja.

Bwana Da Silva  vilevile amebaini kuwa katika mwaka wa 2016,duniani kote, kulikuwa na takriban  watu millioni 66 waliolazimishwa kuacha makazi yao na karibu millioni 25 walitoka  katika nchi tano zinazokabilana na migogoro katika eneo la Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Kipaumbele cha FAO.

Amesema suala muhimu ni kusaidia nchi kufanikisha lengo namba mbili la malengo ya maendeleo endelevu SDGs linalolenga kuondoa njaa  pamoja na matatizo yanayosababisha utapiamlo sambamba ba kukuza kilimo endelevu.