Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulizi yahusianayo na uchaguzi Afghanistan yachukiza-UNAMA

Tadamichi Yamamoto, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan
Picha ya UN /Eskinder Debebe
Tadamichi Yamamoto, Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan

Mashambulizi yahusianayo na uchaguzi Afghanistan yachukiza-UNAMA

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umesema mashambulizi dhidi ya maeneo yanayohusika na masuala ya uchaguzi nchini Afghanistan yanachukiza.

Tamko hilo linafuatia mfululizo wa maeneo hayo ikiwemo vituo vya kusajili wapiga kura wakati huu ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UN nchini humo Tadamicho Yamamoto amesema tangu kuanza kwa uandikishaji wapiga kura tarehe 14 mwezi huu raia 271 wameuawa katika matukio 23.

Amesema idadi kubwa ya wahanga ni katika tukio la tarehe 22 mwezi uliopita ambapo raia 198 waliuawa kwenye kituo cha kugawa kadi za uraia mjini Kabul.

Yamamoto ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA amesema anachukuzwa sana na vitendo vya kushambulia raia kwa makusudi, raia ambao wanasaka kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.

Katika ripoti yake, UNAMA ikipatiwa jina mashambulizi yahusiana na uchaguzi na kipindi cha usajili wapiga kura, imesema asilimia 75 ya mashambulizi yamefanyika kwenye shule au misikiti kwa lengo la kuwajenga hofu raia wanaotaka kupiga kura.

Amesema ghasia hizi lazima zikumbushe kila mtu kuwa juhudi za kuleta amani nchini humo haziwekwi kuwekwa Kwando na kwamba mwelekeo si kusaka suluhu ya kijeshi bali mchakato wa kidemokrasia.

Amerejelea wito wake kwa watalibani kukubali pendekezo la Rais Ghani la kushiriki uchaguzi na kuanza mazungumzo ya amani na serikali ili kumaliza machungu wanayopata raia wa Afghanistan.

Mkuu huyo wa UNAMA amesema Umoja wa Mataifa umejizatiti kuendelea kusaidia mchakato wa uchaguzi Afghanistan.