Tanzania yavalia njuga uhifadhi wa misitu

10 Mei 2018

Tanzania imesema inasimamia kidete suala la uhifadhi wa misitu.

Kauli hiyo ni kwa mujibu wa Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Mkurugenzi wa misitu na nyuki katika Wizara ya maliasili na utalii nchini Tanzania.

Akihojiwa na Idhaa hii kando mwa jukwaa la 13 la misitu linaloendelea jijini New York, Marekani Dkt. Mwakalukwa amesema ni kwa kuzingatia hilo ndio maana wanashiriki jukwaa hilo ambalo..

(Sauti ya Dkt. Ezekiel  Mwakalukwa)

Na kuhusu hatua ziliyopigwa na Tanzania katika uhifadhi wa misitu kufuatia malengo yaliowekwa na Umoja wa mataifa kuhusu ulinzi wa misitu duniani, Dk Mwakalukwa amesema..

(Sauti ya Dkt. Ezekiel  Mwakalukwa)

Mkutano huo unaotarajia kukunja jamvi kesho unazungumzia mikakati iliyowekwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa  kuhusu uhifadhi wa misitu kama njia pekee katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo mara nyingi husababishwa na uharibifu wa mazingira pamoja na ukataji miti kiholela.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud