Amani ya Darfur iko mikononi mwa watu wa Darfur na serikali yao:Ngondi

10 Mei 2018

Maendeleo na amani ya kudumu katika eneo lililoghubikwa na mizozo la Darfur nchini Sudan  vitaletwa na raia wenyewe wa Darfur pamoja na serikali ya nchi hiyo.

Hayo yamesemwa na kamanda wa kikosi cha pamoja cha Muungano wa Afrika AU na Umoja wa Mataifa cha kulinda amani Darfur,  UNAMID, Luteni Jenerali Leonard Ngondi, mjini New York Marekani kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa  akihudhuria vikao vya masuala ya ulinzi wa amani. Ngondi ameongeza

(SAUTI YA GEN NGONDI)

Kikosi cha UNAMID  kilianza kazi zake rasmi Darfur Disemba 31 mwaka 2007 na  muda wake unamalizika Juni mwaka huu. Shughuli ya kuondoa vikosi vya UNAMID imeshaanza na kamanda Ngondi anaeleza ilipofikia

(SAUTI YA NGONDI)

Pamoja na mafanikio yaliyopatikana changamoto bado zipo na hivi juzi tu kumeripotiwa  mapigano mapya Jebel Marra. Je anaamini kuwa wanaondoka na kuacha kila sehemu ya Darfur ikiwa salama?

(SAUTI YA NGONDI)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter