Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uturuki ondoa hali ya dharura – Zeid

Picha na UM
Bendera ya Uturuki:

Uturuki ondoa hali ya dharura – Zeid

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umetaka Uturuki iondoe hali ya dharura wakati huu ambapo wananchi wanajianda kwa uchaguzi.

 

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye chombo hicho, Zeid Ra’ad Al Hussein amesema hali hiyo iliyotangazwa na Uturuki mara 7 ndani ya miaka miwili sasa imesababisha kuzorota kwa hali ya haki za binadamu nchini humo.

Mathalani amesema zaidi ya waandishi wa habari 29 wamekamatwa kwa tuhuma za ugaidi, wananchi wanaishi kwa hofu kubwa  huku uhuru wa kujieleza na kukusanyika ukibinywa.

Bwana Zeid amesema hali hiyo dharura inakiuka tamko la haki za binadamu kuhusu haki za kisiasa na kiraia akitaja vifungu namba 19,21, na 22.

Ofisi ya haki za binadamu imekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya dharura Uturuki kufuatia jaribio la kumuondoa madarakani Rais Recep Tayyip Erdoğan tarehe 15 mwezi julai mwaka 2016, tukio lililosababisha kutiwa korokoroni kwa viongozi wa ngazi ya juu jeshini, wanahabari na wanasiasa.