Lindeni wahamiaji-IOM

8 Mei 2018

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wahamiaji IOM lina wasiwasi kutokana na hali mbaya ya wahamiaji  nchini  Yemen.

 

Wasiwasi huo umetolewa na  mkuu wa operesheni na masuala ya dharura katika shirika hiloMohammed Abdiker mjini Sana’a Yemen baada ya kushuhudia hali ya wahamiaji.

Msemaji wa IOM,Joel millman amewaeleza waandishi habari mjini Geneva leo amenukuu Mohamed Adiker aliyosema

(Sauti ya milliman) 

Amesema kuwa  Mwezi Agosti mwaka jana  ulimwengu ulishtushwa  wakati vijana kadhaa, raia wa Ethiopia na Somalia,  waliolazimishwa kujitosa baharini na wasafirishaji haramu karibu na mwambao wa Yemen na baadae kupoteza maisha yao.”.

Ameongeza kuwa kisa hicho hakikusababisha hali ya kuimarisha ulinzi kwa vijana wengine ambao wana ndoto  ya kupata mazuri wakiwa mbali na kwao na njia  pekee ya kufikia ndoto hizo ni kupitia njia hatari.

(Sauti ya milliman)

“Inakadiriwa kuwa  takriban wahamiaji 7,000 huingia Yemen kila mwezi ambapo idadi ya wote walioingia huko mwaka wa 2017 inakaribia 100,000. Wengi huwa na nia ya kwenda katika mataifa ya Ghuba sanasana Saudi Arabia.”

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter