Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yafurusha zaidi ya 11,00, na vijiji vyachomwa Darfur

Mwanamke huyo na mtoto wake waliokoka chini yamkokoteni yao ni miongoni mwa maelfu ambao wamekimbia vurugu na sasa wamehifadhiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al Salam, Darfur Kusini (maktaba).
Photo: Albert Gonzalez Farran/UNAMID
Mwanamke huyo na mtoto wake waliokoka chini yamkokoteni yao ni miongoni mwa maelfu ambao wamekimbia vurugu na sasa wamehifadhiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al Salam, Darfur Kusini (maktaba).

Machafuko yafurusha zaidi ya 11,00, na vijiji vyachomwa Darfur

Amani na Usalama

Takriban watu 11, 500 wamelazimika kufungasha virago na kukimbia nyumba zao kufuatia machafuko kwenye mji wa Rokero eneo la Jebel Marra jimbo la Darfur nchini Sudan.

Kwa mujibu wa mpango wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika nchini Sudan UNAMID, machafuko hayo yalizuka mwezi April kati ya makundi mbalimbali yenye silaha.

Idadi hiyo ya waliotawanywa ni ya makadirio ya awali yaliyofanywa na timu ya tathimini iliyojumuisha mashirika mbalimbali yaliyozuru eneo hilo hivi karibuni.

Vijiji kadhaa viearifiwa kuchomwa moto wakati wa machafuko hayo, na wengi wa watu wapywa waliotawanywa hivi sasa walishawahi kutawanywa siku za nyuma na machafuko mengine.

Baada ya kuzikimbia nyumba zao watu hao sasa wanalala chini ya miti na wanahitaji haraka msaada wa chakula, malazi, maji na vifaa vya kujisafi. Kata nzima ya Jemeza katika mji wa Rokero ina pampu moja tu ya maji inayofanya kazi kwa ajili ya kuwahudumia watu 15,00 na hakuna kituo chochote cha afya.

UNAMID inasema wiki iliyopita jumla ya watu 1,900 wakiwemo watoto, kina mama wanaonyonyesha na wajawazito walipatiwa msaada lakini maelfu badohawajapata msaada wowote.