Changamoto za maji, uchafuzi wa mazingira na majanga zinahitaji takwimu na usimamizi: WMO
Mkutano wa kimataifa kuhusu kiwango, ubora na usambazaji wa huduma za maji yatokanayo na vyanzo mbalimbali ( Hydro Conference) umeanza leo mjini Geneva Uswis kwa lengo la kushughulikia mhitaji ya haraka ya kuboresha utabiri, udhibiti na matumizai ya rasilimali za maji katika karne hii iliyoghubikwa na changamoto za maji, uchafuzi wa mazingira na majanga kama mafuriko.
Mkutano huo wa siku mbili utakaomalizika May 9 pia na kusanya wadau kutoka kila pembe ya dunia unataka kuanzisha ushirikiano bora kati ya watoaji huduma za maji na watumiaji ambao wanahitaji huduma hizo kwa ajili ya kufanya maamuzi mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa jamii.
Kwa mujibu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO ambalo ndio waandaji wa mkutano huo mambo matatu muhimu yanayotiliwa mkazo ni, mosi kuchagiza ushirika kwa ajili ya miradi mipya na inayoendelea ikiwepo kuanzisha utaratibu wa kubadilishana takwimu, pili kutumia ujuzi na utaalamu wa wadau mbalimbali wa maji ili kuratibu jitihada za athari kubwa na tatu Kuhamasisha viongozi wa sekta ya umma na binafsi ili kuendeleza msaada kwa ajili ya mipango muhimu ya rasilimali za maji.
Maria Helena Ramos ni mtafiti wa sayansi ya hali ya hewa na masuala ya maji kutoka taasisi ya kitaifa ya Ufaransa lakini pia ni rais wa jumuiya ya sayansi ya masuala ya maji kwenye muungano wa Ulaya ameongeza kuwa
(SAUTI YA MARIA RAMOS)
“Inaonyesha jinsi gani maji yanaingiliana na malengo yote ya SDG’s , mafuriko ambayo yamekatili maisha ya watu wengi au ukame ambao unaendelea kwa miongo katika baadhi ya nchi , pia mabadiliko ya tabia nchi , hivyo nchi zinahofia ni jinsi gani tunaweza kushirikiana rasilimali hizona jinsi gani tunaweza kuhakikisha kwamba tuna maji yenye ubora nay a kutosha kwa ajili ya shughuli zetu, watu wetu na shughuli zetu za kiuchumi.”
Inakadiriwa kuwa ifikapo 2015 mtu mmoja kati ya wanne ataishi kwenye nchi ambayo imeathirika na tatizo sugu la ukosefu wa maji , na athari za mafuriko zinakadiriwa kuwa ni dola bilioni 120 kwa mwaka na athari za ukame zitadumaza ukuaji wa uchumi.
Katibu mkuu wa WMO Petteri Taalas ametaja ssababu kuu zinazochangia changamoto za maji duniani kuwa ni ongezeko la idadi ya watu , ukuaji wa miji na uchafuzi wa mazingira.