Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake warohigya: Baada ya kubakwa sasa ni wajawazito

Kijana waRohingya akibeba kuni kichwani katika Cox's Bazar. Inasemekana wanawake na wasichana walibakwa nchini Myanmar walikotoroka
Picha ya UNICEF/UNO20454/Sokol
Kijana waRohingya akibeba kuni kichwani katika Cox's Bazar. Inasemekana wanawake na wasichana walibakwa nchini Myanmar walikotoroka

Wanawake warohigya: Baada ya kubakwa sasa ni wajawazito

Wanawake

Idadi kubwa ya wanawake na wasichana 40,000 wakimbizi wa kirohingya ambao ni wajawazito hivi sasa, walipata hali hiyo baada ya kubakwa.

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa Andrew Gilmour amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya UN jijini New  York, Marekani baada ya ziara yake huko Cox’s Bazar nchini Bangladesh ambako wanaishi wakimbizi hao.

Bwana Gilmour amesema hivi sasa wanawake hao wanakaribia kujifungua lakini katika mazingira magumu na zaidi ya yote..

 (Sauti ya Andrew Gilmour)

“Maelfu wengi waliuawa, wengi wametoweka, lakini pia na waathirika wa unyanyasaji wa kingono nao ni wengi. Ni wengi mno na tunaamini ni kama kuliwa na kampeni ya ukatili  wa kingono”.

Gilmour ambaye ni Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kinachowatia hofu zaidi ni kutokuwepo kwa huduma za afya ya uzazi ikiwemo njia salama za kutoa mimba.

(Sauti ya Andrew Gilmour)

 “Kwa mara nyingine tena hatufahamu ni wanawake wangapi pamoja na wasichana  walio na mimba kwa sasa. Tumesikia taarifa tu kuwa kumetokea visa vya wao wasichana kujaribu kutoa mimba hizo wakwiemo watoto wa kike wenye umri wa miaka 14.”

Akiwa Cox’s Bazar kati ya tarehe 2 hadi 4 mwezi Machi mwaka huu, Bwana Gilmour pamoja na kuzuru kambi zinazohifadhi wakimbizi hao wa Rohingya kutoka Myanmar, alipata fursa pia ya kuzungumza na wale waliowasili eneo hilo hivi karibuni.