Wakazi Bangui tulieni- MINUSCA

2 Mei 2018

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umesihi wananchi kuwa watulivu  kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na kikundi cha wahalifu kwenye viunga vya mji mkuu, Bangui.

Mapigano yameripotiwa kati ya pande mbili hizo yaliripotiwa kwenye eneo la Fatima baada ya wafuasi wa kikundi kimoja cha uhalifu kutiwa mbaroni na vikosi vya usalama.

Taarifa ya MINUSCA imesema kufuatia tukio hilo, walinda amani wa ujumbe  huo walipelekwa ili kuimarisha doria kwenye maeneo ya Bangui.

Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, msemaji wa MINUSCA Vladmir Monteiro amefafanua tukio hilo.

(Sauti ya Vladmir Monteiro)

“Hali leo ni shwari ikilinganshwa na tukio la ghasia lililotokewa jana katika wilaya ya Tatu ya Bangui, karibu na kanisa.  Baadhi ya raia wamepoteza maisha yao na wengine wamejeruhiwa na hii leo Waziri Mkuu amewatembelea kuwajulia hali yao.”

MINUSCA imerejelea msimamo wake kuwa ni vikundi vya serikali vilivyopatiwa mamlaka ndiyo vyenye uwezo wa kusimamia haki na kwamba kikundi chochote cha kiraia kisicho na mamlaka hakipaswi kujichukulia sheria mkononi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter