Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila nishati endelevu wanawake Malawi wataendelea kuteseka- Chavula

Picha:2006 © UNEP
Matumizi ya kuni kwa ajili ya nishati ya kupikia ni moja ya sababu za mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa mazingira. (Picha:2006 © UNEP)

Bila nishati endelevu wanawake Malawi wataendelea kuteseka- Chavula

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Athari zitokanazo na matumizi ya nishati isiyo salama hususan wakati wa kupikia ni moja ya kichocheo cha kuandika makala iliyonipatia ushindi wa tuzo. Amesema James Chavula mshindi wa tuzo ya Voice of Brighter Future. 

Tuzo hizo zimedhaminiwa na Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya usaidizi kwa nchi zenye uchumi duni.

James kutoka Malawi na washindi wengine 6 wanakabidhiwa tuzo hizo kesho Mei 3 huko Lisbon, Ureno, siku ambayo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, ambapo makala yake ya “Smoky kitchens: Malawi’s cooking crisis” ndiyo imemwezesha kushinda tuzo.

Nilizungumza na James na akanieleza sababu ya yeye kuandika makala hiyo inayohusu watu wa kipato cha chini  hususan wanawake.

(Sauti ya James Chavula)

“Nimekulia katika familia ya  kawaida, ambako watu hutumia kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia. Nimeshuhudia wanawake wakitoka majiko huku macho yaao yakiwa mekundu, wakikohoa na kupiga chafya.Asilimia kubwa ya wanawake nchini Malawi huamka alfajiri kabla wanaume na kutembea umbali mrefu kutafuta kuni.

Na kuhusu athari  za kimazingira na kiuchumi zinazotokanazo na matumizi ya kupindukia ya kuni , katika jamii ya watu wa Malawi Bwana James anasema……

(Sauti ya James Chavula )

“Moja ya athari  ni kwamba  kutokana na matumizi ya kupindikia ya kuni na mkaa  kila unapokwenda nchini Malawi  utakuta kwamba misitu inatoweka kwa haraka kuliko tunavyopanda miti. Kila unakokwenda unakuta mifuko ya mkaa imezagaa. Na pili ni kwamba kwasababu tunategemea misitu kuzuia mafuriko. Sasa katika uzalishaji wa umeme tunashuhudia maji yakipungua  na yanapopungua maji umeme unaozalishwa kwa maji unakuwa wa mgao, wakati mwingine tunalala saa 12 bila umeme.”